Tom Boy Mke Mwenza Season 2
Alinitizama huki akitabasamu. kisha akanij...
Alinitizama huki akitabasamu. kisha akanijibu, tena akiwa anazama chumbani.
"Kawthar cha ajabu ni nini? Ili hali mimi na wewe tuna share, na tunaweza kulala kitanda kimoja na mme wetu" kabla hajaendelea nilimkatisha.
"Zaonab naomba utoke chumbani kwangu, nafkiri nyumba ina vyumba vingi hatuna haja ya kugomba" niliongea lakini wakati huo kichwa kilikuwa kinaniuma, mawazo yalinizidia nilitamani kupewa nafasi nipumzike angalau kichwa kipate mwanga mpya.
Lakini kabla Zainab hajajibu chochote Ibrahim aliingilia kati.
"Kawthar na Zainab naombeni mketi tuongee" hii ilinikwaza hivi kweli kwa hii hali ya leo ni ya kuniambia nitulie ðŸ˜, niliona kweli nilikuwa sahihi tu kuwachukia wanaume, sikujibu kiti zaidi ya kukaaa kitandani, na wote wakakaa hapo hapo na kulikuwa na sofa kubwa tu lingewatosha.
Niliamua kutulia nisipinhe chochote wala kuuliza chochote zaidi ya kunyamaza tu, Ibu alianza kwa kusema.
"Kawthar mke wangu na Zainab naomba mnisikilize, ninyi wote ni wake zangu, nawaheshimu nyote, hakuna anaemzidi mwenzie, sitopenda kuona kelele,kila mtu asimame kwenye nafasi yake na sio kufatiria nafasi ya mwingine, leo hatukuandaa chumba lakini sio sawa tukilala wote, naomba Zainab utalala kwenye chumba kiko huko juu nitakuonesha hakina tatizo na ndio kitakuwa chumba chako, na kuhusu zamu naomba mpange kuanzia kesho, ama tulijadili hili sasa ili kunapokucha hii mada iwe imeisha" sikumuelewa Ibra niliona kama anachukulia kwa udogo sana alichokifanya, sikutaka kujibu ila Zainab akajibu.
"Mme wangu, nilikuwa nashauri kwa leo sio mbaya tukilala tu hapa, muda umeenda kushuka tena, lakini kuhusu zamu nafkiri natakiwa kuanza mimi mgeni, tufanye siku tatu tatu au unaonaje mke mwenza?" Aliniuliza kama kunikebehi, nilijibu kifupi.
"Sawa" lengo yaishe kwa muda huo nipate kulala kwanza.
"Kama wote tumekubaliana, naomba Zainab kama nilivyosema zamu itaanza kesho leo naomba uende kwenye chumba chako nahitaji kuongea na mwenzio" aliongea Ibrahim.
Kwa muda mfupi alinifanya nihisi ni mwanaume bora, lakini kumbe ni wale wale ðŸ˜.
Sikutaka kuongea chochote, Zainab alitoka na Ibrahim ili kupelekwa huko chumba chake kilipo, walivyotoka tu nilizima simu nikafunga mlango ili akija asiweze kuingia, kisha nikaingia bafuni nikalia kwa muda sikujua kama kaja ama hakuja nilikuwa kwenye msongo mmoja mbaya sana wa mawazo ðŸ˜.
Niliwaza ninamkosi na mahisiano, mahisiano yangu ya kwanza rafiki yangu aliniibia, nikapitia maumivu makari kiasi cha kuamua kuwa Tom boy ðŸ˜, sijakaa sawa mtu alienipenda kwa dhambi kapata maradhi, kanileta kwa ndugu yake nimeishia kuletewa mke mwingine tena ata wiki kwenye Ndoa sijamalizaðŸ˜, ama nina mkosi 😠nilijiuliza huku nikianza kulia kwa uchungu sana.
Ninakosea wapi mimiðŸ˜ðŸ˜ mbona kila siku ni mimi tu naumizwa, hakuna anaenifkria, sijawai kuiba bwana wa mtu toka kuzaliwa kwangu, kwanini naishia hivi ðŸ˜, nililia nikachoka nikaweka maji kwenye diaba kubwa lilikuwa humo bafuni, nikajaza mpaka juu, kisha nikazamisha kichwa changu chote ndani ya maji mpaka usawa wa shindo, sikutaka kutoa.