Tom Boy Mke Mwenza

Tom Boy Mke Mwenza

Kama huendi kanisani, toka nje nifunge mla...

Chapters
Chapter 1

Kama huendi kanisani, toka nje nifunge mlango wangu, siwezi kuacha shetani ndani kwangu akati naenda kukemea mashetani wengine huko", nilisikia kwa mbali sauti ya mama angu akiniamsha na mabango juu, apo nina usingizi wa kutosha na huko kanisani sikuwa na wazo kabisa la kwenda, dah! Nilijua wazi hii kesi kwa mama angu sio rahisi, apa nisipofanya anachokitaka atanitimua na panga 🤣, niliamka nikavaa nitoke, nikashinde mtaani uko mpaka watoke kanisani.

Mama alivyoniona tu akasonya, sikujali nikatoka zangu nje kabisa, naona dada zangu na kaka angu wamevaa kikanisa, mimi ni watatu kuzaliwa kati ya watoto sita, nyumba nzima mimi ndo naonekana shetani la kutisha, kisa tu ni tom boy, basi bwana nishazoea, sijali wala nini, niliondoka nikarudi mida ya mchana, apo washatoka kanisani, nakuta dada angu na mdogo wangu tunaefatana wanajadili mambo yao, mama alibaki kanisani kwa kikao.

"Dada yani yule mjeda ni mpole, adi raha, ni yatima huwa anatamani sana na yeye angekuwa na wazazi namuonea huruma maskini sijui nimkubalie tu" nilivyosikia tu mdogo wangu Rehema anavyojimaliza, kwanza nikacheka kwa nguvu wasikie kisha nikadakia mazungumzo japo hayanihusu.

"Rehema mdogo wangu, nakushauri sijawahi kukushauri wala kukuingilia kwenye mambo yako ila kwa hili ntakushauri, usithubutu ata kwa bahati mbaya, mjeda, mpole, yatima 🤔, nakuapia ukijichanganya ndo utajua kwanini Mungu alimfanya yatima, na ni kwanini umemkuta single singular, huyo kaa nae mbali hana hisia uyo ni zaidi ya Idd amini anaweza kukunyonga uku anakutazama na asihisi chochote cha ajabu, atakufanya u Google namna ya kupona mapenzi" kabla sijaendelea dada angu Leah akadakia.

"Huna cha kumshauli, kama unaweza kumkosoa Mungu kwa kukuumba mwanamke, unalazimisha kuwa mwanaume, unajua nini kuhusu wanaume wewe?" Nilimtizama kwanza ni dada angu ila kayataka nikiongea apa ataanza kulia nilijibu simple tu.

"Da Lea, siwezi kubishana na mtu ambae hajawahi kunyamazishwa na kiss, yani vitu vingi hujawai fanyiwa, mtu unanyamazishwa na kofi 😏, unataka nijibizane na wewe, kuna lipi unaelewa kuhusu malavidavi😏, ushazoea kuteseka usimponze na dogo" niliongea nikaacha analia nikaingia zangu ndani, kama kusikia ashasikia kazi kwake kuchagua cha kufata, huyu dada angu ndo naemfata kaolewa ila sasa mmh, kaolewa kama sifa tu ya ndani kwake yanatisha.

Kidogo mama akaja, kafika kaanza kunisema, nikaona hapa nisepe nisije kupewa laana buree, nilitoka uzuri tulikuwa tumeshakula, nikaenda kwa demu wangu, nikashinde huko, nikiwa ata sijafika nakutana na mmama ni family friend wetu, akanisimamisha, nikamsalimia akaanza 🙌.

"Recho binti yangu, naomba twende nyumbani ninamaongezi na wewe", dah kwanza aliniboa ananiitaje mimi binti yake how?, nilijikaza kwa sababu namuheshimu hajawahi kunifanyia chokochoko, na wakati nimefukuzwa kazi kisa ni Tom boy yeye ndo alinipa mtaji wa biashara, na mpaka saivi nina bishara kwa sababu yake, mimi sio ombaomba najihudumia, kutoka home ni kwa sababu tu nilitishiwa laana na najua zipo, sikutaka kujichanganya dhambi nilizonazo zinatosha sitaki kuongeza nyingine.

Ilibidi tu nikubali, tulienda mpaka kwake, akaniomba samahani kama atanikwaza ila anaomba nimsikilize, nilikubali.

"Recho binti yangu, unaweza kuniambia kwa nini umechagua kuwa tom boy, nini kimepelekea wewe kupenda kuwa tom boy?" Dah hili swali lilikuwa zito na kuna namna ilikuwa ngumu sana kulijibu, hakuna mtu aliwahi kuniuliza kwa nini mimi ni nimeamua kuwa Tom boy? hata familia yangu zaidi tu walikuwa wakinilaumu na kunigombeza bika kujua nini napitia, na imekuwaje?, lakini mtu baki ameniuliza tena bila kunilaumu, nilitamani kulia ila nikakaza mimi ni mwanaume sio mwanamke siwezi lia kizembe natakiwa kuwa imara, kwanza nilimtizama kwa kumkazia kisha nikatafakari cha kumjibu, lakini kabla ata sijamjibu wakaingia watoto wake, na tunajuana, ilibidi tukaushe mada yetu kwa sababu ni wageni wanamuda hawajamtembelea mama yao, niliaga na kuomba ntakuja siku nyingine kumjibu swali lake, nikatoka zangu huyo, kwa demu wangu, alikuwa ni mtoto wakishua ila kakamatika kwangu vibaya mno, nilifika akanipokea akiwa analia nikashangaa nani tena kaniharibia furaha yangu🤨, nilikasirika nikamuomba aniambie aliemkasirisha apo nishajiandaa kwenda kulianzisha kwa yeyote, alinikumbatia huku ananiambia tatizo.

"Rock" nilibadilisha jina langu badara ya Recho nikajiita Rock, aliendelea kuniambia.

"Rock kaka angu kajua kama nadate na wewe anataka kuniozesha" aisee nilipanick nikamtuliza kwanza Hanipha wangu, wakati tunaendelea na yetu, kaka mtu akaingia, kwanza akanitandika nilipigika vibaya mno, japo nayeye nilimuonja, ila sio kama mimi, Hanipha alikuwa analia tu akiomba tuache, lakini hakuna aliekuwa anaelewa, kaka mtu alinitizama kwa hasira, na nikaona nguvu zinaniisha nikampiga ya kwenye mayai yake, aliachia ukelele mkubwa, nilikuwa nahasira nae vibaya mno, nilivyoona anaugulia maumivu nilimtandika makofi manne ya nguvu, kisha nikaondoka bila kuaga Hanipha alikiwa ananiita ata sikutaka kumsikiliza nikasepa, mimi na kaka ake tunajuana na sikujua kama ni kaka ake ile kitu ilinitia hasira zaidi yani kumbe nadate na ndugu wa Muddy!!! Yani nilitembea njia nzima natetemeka kwa hasira, nikiwa njiani nahasira zangu nikakoswa koswa na gari, alietaka kunigonga akatoka, aisee naona leo sio siku nzuli kwangu, ndo mana nakutana na matatizo tu mtu kavaa mavazi yakutisha dah....