SHUJAA ALIYEDHARAULIKA

SHUJAA ALIYEDHARAULIKA

Ilikuwa ni Siku ya Jumatatu mida ya jioni,...

Chapters
Chapter 1

Ilikuwa ni Siku ya Jumatatu mida ya jioni, kijana aliye julikana kwa jina la kambona alionekana akiwa anarudi shuleni huku uso mzima ukiwa umechora alama za makofi na makalio yake yameiva kwa alama za viboko. kambona alikuwa anatembea huku macho yake yakiwa mekundu na sura yake ikiwa imepauka kwa michirizi ya machozi yaliyo kaukia. hiyo ilikuwa ni uthibitisho tosha Kwamba kijana huyo kalia mpaka kilio Cha mwisho na machozi ya kutosha yamemtoka.
Kambona akiwa na kidumu chake mkononi huku mfuko wa daftari ukiwa mkono mwingine Mara alianza kusikia makelele ya kutosha yasiyo eleweka yanatokea wapi.

Kambona kwanza alisimama ili kusikiliza kelele hizo zinatokea wapi na ni kelele za nini haswa. kijana huyo akiwa anazungusha macho huku na kule Mara kwa mbali aliona moshi mkali mno ukiwa unasambaa juu ukiwa unatokea chini. kwa majibu ya haraka haraka yasiyo hitaji vipimo hiyo ilijitosheleza kujaza majibu kwamba kuna kitu kinaungua moto. ila kwa wakati huo kambona hakuelewa ni kitu gani haswa kinaungua Moto.

Kambona alizidi kusonga mbele huku akiwa bado anaushuhudia ule moshi kwa juu, ila tayari kijana huyo maswali mengi yalikuwa yameanza kupita kichwani kwa sababu moshi huo ulikuwa unatokea Maeneo ya kwao. ilikuwa ni ngumu kuthibitisha kwamba ni kwao kwa sababu ya miti ya miembe ambayo ilikuwa inamzuia kijana huyo.

Kambona baada ya kutembea mita kadhaa mbele na kukaribia Nyumbani kwao alishangaa kuona umati mkubwa wa watu wakiwa wamejazana pale kwao huku wakiwa wanapiga makelele. vigeregere na vifijo kwa wingi kana kwamba ni watu wanao shangilia ushindi.
Siyo makelele wala vifijo vilivyo fanya kijana kambona adondoshe kidumu na daftari chini. bali ni ule moto ambao ulikuwa umetanda kwenye nyumba yao ambayo ilikuwa ni nyumba iliyo ezekwa kwa nyasi.

"Bibiiiiii!!!!" Kijana kambona kwa sauti aliita na kuanza kukimbilia pale kwao huku daftari na kiguduria chake vikiwa havina nafasi katika mwili wake kwa wakati huo. maana aliamu kuviacha pale pale chini.

"Oya kinda wake huyo kamateni!!"

"Kama vipi naye aunganishwe na Bibi yake!"

"Rushieni kwenye Moto huyo, maana samaki mmoja akioza wote wanaoza"

"Aaaaa!! Jamani huyo mtoto muacheni!!"

"Hana lolote huyo muacheni jamani ila hatumtaki hapa kijijni"

Hayo yalikuwa ni majibishano ya raia wao kwa wao Mara baada ya kumuona kijana kambona akiwa anakuja kwa kasi.
Mbio za kijana kambona zilienda kuishia mikononi mwa raia, huku wakiwa wamemtuliza chini ya ulinzi.

"Jamani Bibi yangu!? Bibi yangu yuko wapi!?" Kambona akiwa analia kilio kilicho onekana kuwafurahisha wengi aliuliza.

"Bibi yako kachomwa moto kwa sababu hana sifa ya kuishi katika Kijiji hiki, maana ni mwiko wachawi kuishi" Hilo ni jibu ambalo lilifanya kambona hata kilio kimukauke. kwikwi tu zilianza kusikika huku mapigo ya moyo yakiwa yanamuenda sipidi.

"Jamani Bibi yangu, namtaka Bibi yangu! Bibi yangu Mimi, namtaka Bibi yangu" kambona akiwa anatetemeka aliongea sauti ya kwikwi tena kwa machungu. baada ya dakika kama tatu mapigo ya moyo wa kambona yalizidi uwezo wa mwili hatimaye kijana alizimia pale pale.

Baada ya tukio hilo kila mwanakijiji aliye hudhuria Maeneo hayo kufanya tukio aliondoka eneo hilo huku moyo wake ukiwa umesuuzika kwa sababu Imani ya wengi ni kwamba walikuwa wamemuondosha mchawi gwiji pale kijijni ambaye ndo Bibi yake na kambona.

Kambona ni nani haswa!?.....??...

Kijana kambona alikuwa ni mtoto aliye zaliwa kutokana na Mama yake kuingiliwa kimwili na watu wasio julikana pale pale kijijni. miaka kadhaa iliyo pita Mama yake kambona ambaye alikuwa anajulikana kwa jina la Belina akiwa kwenye biashara yake ya kuuza ndizi akiwa anarudi usiku alivamiwa na watu watatu na kuingiliwa kimwili kisha kuachwa.

Kutokana na hali hiyo Belina alijikuta anapata mimba ya bila kupangilia, binti huyo alijaribu kadri awezavyo kutoa ujauzito huo ila ilishindikana. mwishowe aliamua tu kuacha azae ila lengo lake lilikuwa ni kumtupa mtoto baada ya yeye kujifungua tu. maana kwake aliona ni aibu kuwa na mtoto ambaye hana Baba.

Binadamu tunapanga ila Mungu naye anapanga mipango yake, Belina akiwa anapanga mipango yake kumbe Mungu naye alikuwa kapanga mipango yake. baada ya miezi tisa ya kujifungua kufika Belina alipata uchungu akiwa Nyumbani kwao huku msaada wake akiwa ni Mama yake tu ambaye ndo alikuwa kila kitu kwake. kutokana na zile tuhuma ambazo zilikuwa zimezagaa kijiji kizima kwamba Mama yake Belina ni mchawi basi zilifanya Siku hiyo Belina akose msaada kabisa. Mama Belina alihangaika kwa majirani na wanakijiji wengine ilimradi wamsaidie japo baiskeli ampeleke mwanae hospital lakini hakuna aliye mtazama kwa jicho la kumsaidia zaidi ya kila mtu kumrushia matusi mazito.

Mama Belina aliamua kumkokota binti yake mwenyewe kwa nguvu zake ilimladi amfikishe zahanati. ila kabla hajafika popote tayari Belina alifanikiwa kujifungua mtoto wa kiume na baada ya kujifungua Belina alipoteza maisha pale pale na lile lengo lake la kumtupa mtoto lilienda tofauti kabisa.

Hakika Mama Belina aliumia na alilia mno tena kilio Cha uchungu kweli kweli, alitamani amtupe yule mtoto akihisi ndo kachangia kifo Cha binti yake ila aliona haina maana.

Basi Mama Belina kwa kusaidiwa na watu wachache tu ambao Sana Sana walikuwa rafiki zake na Belina walifanikiwa kumzika Belina. na watu wengi waligoma kushiriki mazishi kwa kile walicho dai kwamba Mama Belina ni mchawi.

Basi Mama Belina aliamua kumlea yule mtoto huku akimpatia jina la marehemu mume wake la kambona, kiukweli maisha ya Mama Belina yalikuwa magumu mno na pia alikuwa anatengwa na jamii ila yeye hakuona shida yoyote kwa sababu maneno yote waliyo kuwa wanamsema ulikuwa ni uongo.

Ilipita miaka miwili tangia kambona azaliwe,huku bado Mama Belina akiwa anaishi kwa vifungu pale kijijni, mwishowe maonezi yalizidi vipimo Mama huyo alianza kupokonywa mpaka aridhi ya mashamba yake na viongozi wa kijiji.

Mama Belina alijikaza na yote, maisha yaliendelea, miaka Sita ilikatika mtoto kambona alipelekwa shule na kuanza darasa la kwanza, ila pale shuleni watoto wenzake walionekana wakimsema mno kambona kuhusu uchawi wa Bibi yake, yaani hakuna mtoto ambaye alikuwa anataka kuongea na kambona, na hiyo ilikuwa inatokana na asili ya kijiji hicho kuuchukia uchawi kuliko kitu chochote kile.
Maisha yaliendelea hatimaye kambona alifika Darasa la pili, hapo Sasa mabalaa ndo yalianza maana alianza kuchukiwa mpaka na walimu, yaani shuleni alikuwa anapigwa hovyo bila sababu yoyote, kosa dogo linakuzwa kuwa kubwa.

Huku Nyumbani nako mabalaa ndo yalikuwa yanazidi, Mama Belina hakuacha kufanyiwa visa, ukiwa ni msimu wa mavuno Mama Belina alipo enda shambani kwake alikuta mazao yote yamevunwa bila hata kuelewa aliye vuna.
Siku zote ubaya wa mtu hutengenezwa na watu wenyewe, baada ya Mama Belina kuona Mambo yamemshinda na kila kukicha anapewa tuhuma ya uchawi, aliamua kusafiri na kwenda kijiji kimoja ambacho kilikuwa mbali kabisa, na kijiji hicho kilikuwa kinasifika kwa uchawi haswa, yaani ulikuwa ukitaka uchawi wa aina yoyote ile unaupata.
Mama Belina baada ya kufika huko alikaa wiki moja tu kwa mtaalamu ambaye alikuwa anaaminika, yaani ndani ya wiki moja tu Mama Belina alijifunza uchawi wa kila rangi yaani roho yake iligeuka kuwa roho ya Simba aliyejeruhiwa, yaani alikuwa anafuka tu uchawi popote tu anapo pita.

Baada ya Mama Belina kurudi pale kijijni Sasa matukio yenyewe yenyewe yalianza kutokea yaani ilikuwa siyo kuigiza tena Wala kusingiziwa kama mwanzo, awamu hii alikuwa anafanya kiukweli kweli.
Kwanza Mama Belina alianza na watu walio vuna mazao yake, baada ya wiki moja tu watoto wawili wa mwenyekiti na wengine tu watatu walpoteza maisha pale kijijni kila mtu na staili yake.

Haikupita miezi hata miwili mwenyekiti wa kijiji alipata ulemavu miguu yote bila hata kuelewa ulemavu huo umekujaje, yaani ilikuwa matukio juu ya matukio.

Hapo Sasa chuki baina ya wanakiji na Mama Belina ndo zilizidi kuwa kubwa maana matukio halisia yalianza kutokea tofauti na mwanzo ambapo ilikuwa ni kuhisi tu.

Maisha yaliendelea huku kijana kambona akiwa hajui kama kweli Bibi yake ni mchawi. baada ya miezi kadhaa kambona alipo fika darasa la tatu kuna sakata lilitokea shuleni na kijana huyo alisingiziwa kwamba kaiba pesa karibia laki tatu ya walimu. na yote hiyo ilikuwa ni figisu tu ilimradi afukuzwe shule.

Mama Belina alijitahidi aliuza baadhi ya vitu vyake na kulipa ile pesa ilimladi mjukuu wake aendelee na shule. na kweli ile ilisaidia japo Mateso ya kijana yule pale shuleni hayakupungua.

Baada ya miezi kadhaa mbele kijana kambona alifukuzwa shule kwa sababu ambazo hazieleweki pamoja na kwamba Bibi yake alikuwa kalipa pesa.

Kitu hicho kilifanya Mama Belina apandwe na wazimu moja kwa moja alienda shuleni kutia mkwara na aliwapatia onyo kwamba mjukuu wake akifukuzwa tena basi litatokea Jambo ambalo hawataamini.

Kutokana na dharau za walimu walichukulia poa tu, kesho yake kijana kambona alifukuzwa tena shuleni.

Ilipo fika Jioni tu bila kujulikana imekuwaje hali ya mwalimu kuu ilibadilika na kuwa hali mbaya mno. ambapo ilifanya walimu wenzake wamkimbize zahanati.

Kiukweli Siku hiyo ilipita huku watu wakiwa wameshikilia roho mikononi kuhusu hali ya mwalimu huyo. na tayari kijiji kizima tetesi zilikuwa zimesambaa kwamba Mama Belina kamroga mwalimu kuu muda wowote anapoteza maisha.

Basi Siku mpya ilifika walimu wote walienda shuleni wakiwa na hasira kali, bahati mbaya kwa kijana kambona Siku hiyo naye alienda shuleni bila kujua Kwamba Bibi yake asharikoroga. yaani Siku hiyo pale shuleni kambona aligeuka ndo kipoza hasira Cha walimu pale shuleni, kijana alipigwa kipigo Cha mbwa mwizi, makofi ya kutosha yalipita usoni kwake, yaani asubuhi mpaka Jioni alishinda akipigwa tu.

Wakati hilo linaendelea shuleni, huku mtaani kumbe nako wanakijiji walikusanyika kwenda kufanya tukio kwa Mama Belina na ndo tukio tulilo ona mwanzo. wakati kambona anarudi shuleni na majanga yake ndo kama tulivyo ona mwanzo hali aliyo kutana nayo nyumbani ya Bibi yake kuchomwa pamoja na nyumba.

Baada ya kujua Kwamba kambona ni nani haswa tuendelee....

Baada ya kambona kuzimia watu wote walitawanyika na kumuacha pale pale bila hata kujali lolote.

Kijana kambona alikuja kuziduka kigiza kikiwa kinaanza, na kitu kilicho mfanya ashituke yalikuwa ni manyunyu ya mvua ambayo yalikuwa yameanza kudondoka.

Kambona alipo piga macho mbele ya nyumba aliona kama anaota hivi,kila kitu lilikuwa kimeteketea vibaya mno. basi kijana akiwa hana nguvu huku akiwa anasikia maumivu ya vipigo mwili mzima alisogea pale nyumba ilipo ungua.

Kambona alibaki anatetemeka baada ya kuona mwili wa Bibi yake ukiwa umeungua vibaya mno, yaani miguu ya kambona ilipatwa na ganzi huku mvua kubwa ikiwa imeanza kunyesha.

Huu ni mwanzo wa simulizi ya kusisimua na kutoa machozi kwa wale wenye mioyo miepesi. Ni moja ya simulizi kali za kuburudisha na kuelimisha usikose hata kipande kimoja Cha simulizi hii naamini utanishukuru baadae.