Roho Ya Kutu
Hii ni Hadithi nyingine ya Kutisha na Kusi...
Hii ni Hadithi nyingine ya Kutisha na Kusisimua inayo muhusu kijana Baro na Mama yake walio teseka na kunyanyasika, mpaka kijana Baro Akajikuta anakuwa Mtu wa Roho mbaya kupindukia, mwishowe kujiingiza kwenye ushirikina ulio pindukia! Kama una roho nyepesi na ya Uoga usisome hii hadithi, pia kama una machozi ya Karibu kaa na Leso yako pembeni Kwa ajili ya kupangusa machozi Kwa sababu naamini hii hadithi itakutoa machozi ukiachana na Kukusisimua.
Ila uzuri hadithi hii inaruhusiwa Kwa rika zote Kwa sababu haina matusi.
Mwanzo.
Ni nje ya Mji kabisa kwenye Moja ya kijiji ambacho kilikuwa kipo kilomita kama Kumi kutoka mji ulipo, ndani ya kijiji hicho walionekana wanawake wawili, na mwanaume mmoja wakiwa wanatembea Kwa haraka huku Sura zao zikiwa za chuki na malalamiko.
"Nasema haiwezekani! Lazima tufanye Jambo Dada! Yaani Kessi kafikia hatua ya kumwandika yule mwanamke na mwanae kwenye urithi, Aaaa sikubali!" Hayo yalikuwa maneno ya mwanaume yule wa makamo kidogo Miaka kama 65 hivi,
"Kaka, unajua Mimi na Mama Miano tulilijua hili tokea mwanzo ndo maana tukasema tufanye Jambo ila ubishi wako ndo umetufikisha hapa!" Mwanamke mwingine naye wa makamo kidogo kama Miaka 55 aliitikia.
"Wifi mwambie huyo! Maana kaka yako amekalia ubishi tu Muda wote!" Mwanamke mwingine Miaka kama 60 hivi alidakia!
Watatu hao walizidi kuzungumza Kwa kujilalamisha, baada ya kutembea umbali kadhaa Kwa miguu walikutana na Binti Mmoja njiani akiwa katwisha ndoo ya Maji ilibidi waulize.
"Samahani binti! Tunauliza Kwa mganga anaye itwa! Kirusi maana tumeelekezwa maeneo haya!?" Baba yule ambaye alikuwa kaongozana na wamama wale wawili aliuliza!.
"Hahaaaa!! Haitwi kirusi babu!! Hilo ni Jina la utani kutokana na kazi yake anaitwa Bibi Muweli!" Binti yule akiwa anacheka alijibu!.
"Heeeee inamaana huyo mganga ni mwanamke! Kwani hakuna mtaalamu wa kiume maeneo haya maana wakike siwaamini kabisa!" Baba yule hakurizishwa baada ya kusikia Mganga wanaye muendea ni mwanamke!.
"Babu toa shaka kuhusu huyo Bibi, katika ukanda wote huu yeye ndo mkuu wa hao waganga wengine!" Binti yule alitoa Sifa Kwa huyo Bibi Muweli na maneno yake yalifanya watatu hao waelekee kule waliko elekezwa na kweli baada ya dakika kama kumi walifika Nyumbani Kwa Bibi huyo.
Kwanza mazingira yenyewe palikuwa panatisha isivyo kawaida, kitendo cha kutia tu mguu kwenye yale makazi upepo wa ajabu ulianza kuvuma maeneo yale, gafla walianza kusikia Sauti ya Mtu ikiwa inaongea! Ilikuwa ni Sauti ya Bibi kizee huku ikiwa haieleweki inatokea wapi, yaani ilikuwa ni kama inatokea hewani! Kwanza watatu wale walitumbua macho huku mioyo yao ikiwa imeanza kuponda Kwa kasi kama inataka kuchomoka.
"Vueni Viatu,muingie ndani kinyume nyume huku mkiwa mmefumba macho!" Sauti waliyo sikia ilikuwa inatoa maelezo na ni kweli walifanya kama walivyo elekezwa na waliingia mpaka ndani.
Walikutana na Bibi wa Miaka kama 90 hivi akiwa amekaa kwenye sinia, tena sinia likiwa linaelea angani kimo Cha magoti!.
"Duuuuuu!! Sasa huyu ndo mganga! Yaani hawa ndo wataalamu huwaga nawataka, Sasa Hapa Kessi Kwisha habari yake" Baada ya yule Baba kuona ile Miujiza ya sinia kuelea hewani alijiwazia Kimoyo moyo.
Tuje upande wa huku Mjini ukiachana na huko Kijijini, ni katikati ya Mji ambao ulikuwa umechangamka kiasi chake.
Kwenye Moja ya nyumba ambayo ilikuwa imezungushiwa wigo ikiwa ni nyumba nzuri kawaida, yaani siyo ya kitajiri wala ya kimasikini! Alionekana Baba Mtu mzima Miaka kama 35-40 akiwa kakaa na Mke Wake wanajadili Jambo, ila mwanamke alikuwa anaongea huku akiwa Mtu wa wasiwasi Muno.
"Mama Baro kwani wewe wasiwasi wako ni upi, Mimi nimesema hivi kwenye urithi Wangu wote nimeweka Jina lako na la mwanangu Baro! Wazazi Wangu hawanihusu Kwa lolote na sitabadilisha maamuzi Yangu!" Baba huyo ambaye ndo alikuwa Baba mwenye nyumba aliongea tena Kwa kulalamika.
"Baba Baro Mimi naona hicho kitu siyo kizuri, maana juzi nimekutana na Mama yako maneno aliyo nambia mpaka Naogopa " Mwanamke yule alijibu! Ila mumewe alionekana kasimamia kwenye msimamo wake.
Kwa nini bwana huyu anasema wazazi wake hawamuhusu na kwa nini Yote haya!?? Ngoja turudi nyuma kidogo kuona Historia ya huyu anaye itwa Baba Baro.
Baba Baro Kwa Jina lake kamili anaitwa Kessi! Bwana huyu akiwa ni mdogo wazazi wake walimpeleka Kijijini ili kwenda kuchunga Ng'ombe vibarua ili wao wapate pesa kutokana na Malipo anayo lipwa mtoto wao, wazazi wa Kessi walikuwa na Maisha magumu Muno pale Mjini yaani ndo zile familia tunasema unga unga mwana.
Ni kweli Kessi alipelekwa Kijijini Kwa msukuma mmoja ambaye alikuwa na Ng'ombe Zaidi ya mia.
Kessi alikuwa ni Mtu anaye penda Muno kusoma ila wazazi wake walikataa kata kata kijana huyo kupata elimu yaani familia nzima ilikuwa haitaki Kessi asome, na kijana Kessi yeye alikuwa ni mtoto wa tatu kwenye familia ya watoto kama watano hivi! Huku akiwa katanguliwa na Dada yake na kaka yake japo alikuwa anapishana nao mwaka kama mmoja hivi, na wote hao hakuna hata mmoja ambaye alikuwa anasoma zaidi zaidi walikuwa wanafanya vibarua.
Watoto wengine wanne walionekana kufurahishwa na ile hali ya kuto kwenda Shule na kufanya vibarua ila ilikuwa tofauti Kwa kijana Kessi ambaye alikuwa anapenda Shule.
Kijana Kessi akiwa Kijijini bahati nzuri alikutana na msamalia mwema ambaye aliamua kumsaidia baada ya Kessi kuonesha nia ya kusoma.
Akiwa huko huko Kijijini Kesi aliacha kibarua Cha kuchunga Ng'ombe alianza shule, na Kessi alikuwa anakaa Kwa Mtu huyo ambaye alikuwa hata Siyo ndugu yake.
Kijana Kessi alisoma Shule miezi Sita tu, wazazi wa Kessi walipo pata taarifa kwamba mtoto wao kaacha kazi na kaanza kusoma walikasirika Muno, kwanza Baba yake na Kessi ambaye alikuwa anaitwa Kipao, aliamua kwenda huko huko Kijijini na kumchukua mwanae Kwa nguvu kurejea naye Mjini.
Mpaka hapo masomo ya Kessi yalisitishwa tena, maana baada ya Kessi kufika Mjini ilibidi aanze Kazi ya kutembeza na kuuza Maji ya kandoro huku pesa yote anayo fanya biashara ikiwa inachukuliwa na Baba yake pindi tu akirudi nyumbani Jioni.
Kijana Kessi alikuwa na bahati Muno, katika harakati zake za kuuza Maji alikutana tena na msamalia Mwema kipindi hicho Kessi alikuwa na miaka kama 9.
Kessi alipelekwa Shuleni na huyo msamalia Mwema, ila wazazi wa Kessi walikuja juu muno kuona mtoto wao kapelekwa Shuleni, lakini kutokana na huyo msamalia Mwema kuwa mtumishi wa Serikali alitishia kuwapeleka mahakamani wazazi wa Kessi, hapo ilibidi wawe wapole, Lakini hawakuacha kumpiga Vita ya Chini Chini mtoto wao, mpaka ilifika kipindi Kessi alihama kwao na kuanza kukaa Kwa mwalimu.
Maisha yaliendelea Kessi alimaliza mpaka Darasa la Saba na kufanikiwa kujiunga kidato cha kwanza huku akiwa ni mwanafuzi anaye jitahidi Muno!.
Shangazi yake na Kessi alikuwa ni Mtu wa kuamini waganga tangia akiwa binti, baada ya kuona Kessi anakuwa mbishi aliamua kutumia ndumba na kweli Kijana Kessi aliugua nusura ya kufa mpaka pale alipo pelekwa kwenye maombi na mwalimu ambaye alikuwa anakaa nayee!.
Kessi alimaliza kidato cha nne na alifanikiwa kujiunga na chuo Cha Diploma kwenda kusomea maswala ya uongozi na utawala!, Baada ya wazazi wa Kessi kuona Kijana wao anazidi kutoboa walianza kupata tu aibu huku wakiwa wanachekwa mtaani na watu.
Baada ya Miaka kadhaa Kessi alifanikiwa kumaliza masomo na alipata Kazi kwenye Shirika la Umeme tena akiwa kawekwa kitengo kizuri tu Cha utawala Bora kwenye Shirika Hilo.
Kesi alianza kufanya kazi Kwa bidii huku wazazi wake wakiwa wameanza kujisogeza taratibu taratibu, na kipindi hicho hicho Kessi Alibahatika kupata mwanamke na kumuoa!.
Pia kitendo cha Kessi kuoa hakikuwafurahisha kabisa wazazi wa Kessi Kwa sababu waliona kama wao hawatafaidi vizuri matunda ya mtoto wao.
Kessi wala hakujali, alioa na baada ya Muda kupita walipata mtoto wa kiume ambaye walimpatia Jina la Benni.
Kessi alikuwa hana kinyongo na wazazi wake pamoja na ndugu zake wengine, kile kidogo ambacho alikuwa anapata alikuwa anawasaidia, ila bado ndugu zake walionekana kutoridhika kabisa, yaani waliona kama Mke wa Kessi na yule mtoto mchanga wanapunguza bajeti na kufanya wao wasipate pesa za kutosha.
Shangazi yake na Kessi pamoja na Mama yake walienda Kwa wataalamu kuroga, ni kweli Lengo lao lilitimia, mtoto wa Kessi akiwa na miezi nane tu alifariki tena aliariki bila kuugua, yaani alilala usingizi kawaida na hakuamka tena.
Kessi aliumia Muno na ile hali, na bahati mbaya wale wale ndugu zake walianza kumjaza maneno kwamba Mkewe ndo kasababisha mpaka mtoto anakufa kutokana na uchawi wake!.
Kwakuwa Kessi alikuwa haamini Mambo ya kishirikina alipiga Moyo konde na kuendelea na maisha kama Kawaida!.
Baada ya miezi kadhaa mkewe alipata ujauzito mwingine na miezi ya kujifungua ilipo fika alijifungua mtoto wa kiume na Jina walimuita Baro.
Awamu hii wale ndugu zake na Kessi wakiwepo wazazi wake Dada zake na kaka zake baada ya kuona kizuizi Cha wao kupata pesa za kutosha kutoka Kwa Kessi ni Mke wa Kessi, walipanga njama za kumvamia Mke wa kesi ikiwezekana wamumalize kabisa, Kessi alipo gundua hiyo mbinu huo ndo ulikuwa Mwisho wake yeye na ndugu zake, yaani mahusiano yaliisha pale pale.
Kesi alizidi kuishi na Mke wake na walifanikiwa kujenga nyumba nzuri na kufungua baadhi ya biashara, Kesi baada ya kuona katengeneza Jina kupitia kazi yake aliamua kujaribu kwenye siasa kwa Sababu alikuwa na elimu kuhusu maswala ya uongozi,na aligombea udiwani kwenye kata ya mtaa anao tokea! Na kweli Mungu Siyo Athumani alipata udiwani.
Ndugu zake na Kessi walibaki kujizungusha pembeni na kumchafua Kessi Lakini haikusaidia! Mwishowe walianza kujikomba komba Kwa Kessi maana Katika ukoo wote Mtu mwenye mafanikio walau kidogo alikuwa ni huyo Kessi.
Sasa kizazaa kilianza baada kugundulika kwamba Kessi kaandika wosia endapo lolote litatokea kwake! Watu wakurithi Mali zake ni mtoto wake Baro na mkewe tu na siyo Mtu yeyote!.
Ndugu wa Kessi au Baba Baro kama Jina la mtoto wake lilivyo baada ya kubaini hilo walichachamaa na kuona Sasa masihara yamezidi.
Nadhani tumeona historia fupi ya Baba Baro mpaka tunaona mgogoro na ndugu zake.
Baada ya kujua Historia ya Baba Baro tuendeleee Sasa........
Muda huo Baba Baro anaongea na Mke Wake pale nyumbani, Mara kuna mtoto Miaka kama Saba hivi aliingia mule ndani akiwa kachafuka balaa huku akiwa analia!.
"Baro nilikwambia acha kucheza huo Mpira ona Sasa ulivyo umia!" Mama Baro baada ya kugundua mwanae kaumia alianza kufoka, ila baada ya kumkagua vizuri Baro waligundua Mkono wake umevunjika!.
Haraka haraka Baba Baro au Kessi alichukua pikipiki yake aina ya Boksa ambayo alikuwa nayo na aliwapakiza Mama Baro na mwanae Kwa ajili ya kumpeleka mwanae hospital.
Turudi upande wa pili kule Kijijini tuliko ona wale watatu wanaenda Kwa mtaalamu.
Baada ya madakika kadhaa kupita watatu wale walionekana wakitoka pale Kwa mtaalamu meno yote yakiwa nje ikiwa ni ishara ya ushindi.
"Sasa hapa Kazi Kwisha!" Baba yule Mtu mzima aliongea Kwamizuka haswa.
"Kaka Siyo Mimi nahangaika hivi alafu uje ufike Muda wa kuvuna tuanze kukataana!"
"Aaaaaa Dada usijali! Mambo yakiwa Sawa ile nyumba yake ndogo ya wapangaji pale njia panda utakaa wewe na watoto wako!"
"Hahaaaa msinichekeshe Mimi! Kwa hiyo baba Kessi umeanza kutoa urithi Kabla au Siyo!?" Mke Mtu aliongea Kwa kucheka.
"Alafu Mke Wangu nilikukataza kuniita Baba Kessi niite Baba Miano hilo ndo nalitaka! Kwanza unamzungumziaje marehemu mtarajiwa!" Baba yule aliongea Kwa kufoka kidogo, watatu hao walikuwa ni wazazi wa Kessi au Baba Baro, maana yake walikuwa babu yake na mtoto Baro, wawili walikuwa wazazi wa Kessi na mmoja alikuwa ni shangazi yake na Kessi.
Turudi upande wa Huku Kwa Baba Baro na familia yake, bwana huyo akiwa anaendesha pikipiki yake kuelekea hospital alihisi kama ukungu umepita machoni kwake, akiwa anataka kuminya breki pale pale pikipiki iliingia kwenye mtaro na kula mweleka.
Kuna mengi yanakuja huu ni mwanzo tu wa hadithi je Kwa Nini Hadithi inaitwa Roho ya Kutu!??