Mr Nobody

Mr Nobody

Ilikuwa majira ya asubuhi alionekana kijan...

Chapters
Chapter 1

Ilikuwa majira ya asubuhi alionekana kijana mmoja akiwa na haraka, aliendesha gari lake kwa mwendo wa kasi kidogo huku akiangalia saa yake ya mkononi.
Alifika sehemu ya wa wavuka kwa miguu akataka kupita ikiwa watu wamesimama.
Upande wa kushoto wa barabara kulikuwa na binti mmoja akiwa na kundi la wanafunzi aliokuwa anataka kuwavusha .
Yule kijana alipowaona alifunga break na kuwaruhusu wapite.
Yule binti ( Alina) aliwavusha upande wa pili wa barabara.
Watoto walimuaga kwa furaha.
" Asante , bye dada.
" Bye masomo mema.
Baada ya kuagana na watoto alimfuata yule kijana.
" Wewe kaka upo sawa kweli, huko kwenu hakuna watoto?
Kijana alimuangalia Alina bila kujibu.
" Kuwa makini barabarani na ujitunze kufuata sheria za barabarani. Pia kumbuka hawa ni watoto wanataka uangalizi kutoka kwetu.
" Sawa dada nimekuelewa.
Alina aliondoka akaenda kupanda kwenye gari yake huku yule kijana alikuwa akimuangalia mpaka alipowasha gari na kuondoka.
Kijana alijisahau kama yupo barabarani alisababisha jam huko nyuma alipigiwa honi na wengine walimuongelesha kwa ukali.
Kijana alitabasamu kisha akaanza kuendesha gari.
" Kuna kitu ndani ya huyu binti natamani kumjua zaidi.

Katika eneo la Masaki, moja ya maeneo ya kifahari zaidi jijini Dar es Salaam kulikuwa na nyumba kubwa ya kifahari , ilikuwa ni nyumba ya familia ya Mzee Richard Mwandila.
Mzee Richard alikuwa mfanyabiashara mkubwa aliyemiliki kampuni za ujenzi, hoteli na uwekezaji katika sekta mbalimbali. Jina lake lilijulikana ndani na nje ya nchi.
Mke wake Madam Veronica Mwandila alikuwa mwanamke wa hadhi ya juu aliyependa maisha ya kifahari na kuamini kuwa pesa ndiyo msingi wa kila mafanikio.

Katika familia yao walikuwa na mabinti watatu warembo waliovutia kila walipopita.
Wa kwanza aliitwa Vanessa Mwandila. Alikuwa mrembo, mwenye kujiamini na aliyependa kuonekana katika hafla kubwa za watu wenye pesa pia alikuwa ameolewa na mfanya biashara maarufu .

Wa pili alikuwa Samantha Mwandila. Huyu alikuwa maarufu kwenye mitandao ya kijamii na alifuatwa na maelfu ya watu waliopenda maisha yake ya kifahari pia alikuwa amechumbiwa na mtoto wa waziri.

Wa mwisho alikuwa Alina Mwandila.
Alikuwa tofauti sana na dada zake, Alina alikuwa mtulivu, mwenye huruma na aliyependa kuthamini utu kuliko mali.
Ingawa alikulia katika utajiri mkubwa, moyo wake haukuwahi kuvutiwa na anasa wala ufujaji wa pesa.
Alina alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa mwisho katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, akisomea Shahada ya Mahusiano ya Kimataifa.
Kila siku Alina alienda chuoni kwa gari lake la kifahari aina ya Range Rover alilopewa na baba yake kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa.

Siku moja jioni baada ya kutoka maktaba kuu ya chuo, mvua kubwa ilianza kunyesha ghafla.
Wanafunzi wengi walikimbia kutafuta sehemu za kujikinga na mvua.
Alina naye alijaribu kuwahi kwenye gari lake lililokuwa limeegeshwa mbali kidogo.
Akiwa njiani, kisigino cha kiatu chake kilikatika na kumfanya aanguke na
vitabu vyake vyote vikaanguka chini.
"Aaaaaaa .... alipiga kelele .
Watu waliokuwa karibu walimcheka na wengine walimpa pole.
Alina hakujali alinyanyuka na kujifuta kidogo.
Kabla hajainama kuokota vitabu vyake mara kijana mmoja alifika na kuanza kuviokota kisha akasimama na kusema.
"Pole sana.
Alina alimuangalia.
Kwa sekunde kadhaa.

Huyo kijana alikuwa mrefu, mwenye mwili wa mazoezi na sura yake ilikuwa na mvuto.
Alikuwa amevaa jeans ya rangi ya blue iliyopauka, tisheti nyeusi na koti la mvua.
Kwa kumwangalia tu mtu yeyote angeamini ni kijana wa kawaida anayepambana na maisha.
"Asante.
Alina alisema huku akichukua vitabu vyake.
"Usijali tunaweza kusimama pale kwanza mpaka mvua itakapopungua.
" Sawa
Alina alikubali wakaenda kujubanza
Kwenye kibanda kidogo karibu na eneo la maegesho.
Yule kijana alikuwa muongeaji na mambo mengi alivyoongea yalikuwa ya msingi sana hapo ndipo Alina akagundua kuwa kijana huyo alikuwa na akili nyingi, hekima na unyenyekevu.
"Unaitwa nani?" Alina aliuliza.
"Hansel.
" Ni mwanafunzi?
" Hapana.
"Mbona upo hapa sasa?
Hansel akatabasamu kidogo.
"Natafuta maisha kama watu wengine tu."
Jibu hilo lilimfanya Alina acheke.
Hakujua kwa nini anacheka .
" Maisha ya atafutwa kwa njia nyingi , je wewe inayotafuta kwa njia gani?
Hansel alifikiria kidogo alafu akasema.
" Mimi ni dereva boda, hata kufika hapa nilikuwa nimemleta mteja wangu.
"Sawa ni vizuri kutafuta hela ya halali kuliko kutumia njia za hatari.
" Ni kweli.
" Nimefurahi kukufahamu Hansel, naona mvua imekata acha niondoke sasa.
" Sawa lakini bado sijakufahamu unaitwa nani?
" Ooooh samahani , naitwa Alina.
" Nimefurahi kukufahamu Alina .
" Ok bye.

Alina aliondoka huku Hansel akimsindikiza kwa macho mpaka alipopanda kwenye gari yake na kuondoka.

Siku zilienda Alina na HANSEL walikuwa wanaiona mara kwa mara maeneo ya chuoni.
Taratibu walianza kuwa na ukaribu na wakazozana sana.
Kuna wakati Alina aliacha kutumia gari yake na kutumia pikipiki ya HANSEL.
kadri siku zilivyokuwa zinaenda wawili hawa wakajikuta wameanza kupendana na kuingia kwenye mahusiano.
Alina alihisi amani na furaha ya ajabu akiwa karibu na HANSEL.

Siku moja Hansel alitoka kumrudisha Alina nyumbani kwao alipokuwa anaondoka alipiga simu sehemu.
" Hey Juma njoo home uchukue pikipiki yako ,sitaweza kuja huko kijiweni kwako.
Baada ya hapo aliondoka .
Alienda sehemu moja kulikuwa na jumba la kifahari alipiga honi geti linafunguliwa kisha akaingia.
" Mlinzi alipomuona alicheka .
" Hansel imekuwaje leo?
Hansel alisimamisha pikipiki akashuka na kusogea karibu na mlinzi kisha alitabasamu na kusema
" Musa unaweza kuona kama kituko lakini kinachofanya ni moja ya kujitengenezea maisha yangu.
" Kivipi.
" Tulia ipo siku utajua.
Hansel aliondoka huku Musa akimuangalia alivyovaa nguo zilizopauka na koti kubwa.
" Jamani ndio avae koti kama mlinzi wa kwenye magodauni?

Hansel aliingia ndani kwenye jumba la kifahari, aliingia kwenye moja ya chumba akavua nguo na kwenda kuoga.
Baada ya hapo alivalia kaptula na shati ambalo hakuwa amefunga vifungo, alimimina wine kwenye grass kisha akaenda kusimama kwenye balcony huku akinywa kinywaji chake taratibu.
Mara alikuja kijana ( Juma)
" Oya kaka vipi mbona kama una amani kila kitu kinaenda sawa?