Mr C.E.O Simulizi Ya Mapenzi

Mr C.E.O Simulizi Ya Mapenzi

Nilipo maliza masomo yangu katika chuo kik...

Chapters
Chapter 1

Nilipo maliza masomo yangu katika chuo kikuu cha Dar es salaam (udsm ) ilikuwa changamoto sana kupata kazi,kama mnavyojua hali ya sasa katika sekta ya ajira ilivyo ngumuuuu ,ukipeleka maombi mahali au ofisi fulani utaambiwa "acha maombi tutayashughulikia dada" mmmmhu na kukesha kote kule kusoma jamani,.....na baridi lote lile la bording (kwa waliosoma machame girls) wanajua hali ilivyo baridi kaliiiiiii na unaamka hivyo hivyooo ili usome hasa sisi tuliochukua masomo ya sayansi ndio mkazo ulikuwa zaidi

wakati huo nilikuwa nimepanga na rafiki yangu anaitwa sarah,yeye alifanikiwa kupata ajira mapema tu huyu ni rafiki yangu nilitoka nae high school,hakuacha kunipa moyo hasa na alinibeba mnooo ....thanks sarah

Siku moja mapeema nikapeleka maombi kwenye ofisi moja wapo kuuubwaaa ila moyoni nilijua kabisa sipati😄😄😄 ila ndio hivyo tena kujaribu bahati ,nikafika mapemaa asubuhi pale nikapanda lifti mpka ofisi nilizokusudia .....kiroho kinadundaaaa mi nimuogaaa sanaa nikakuta ndio kwanza secretary anaandaa andaa mambo pale nikamsalimia ,za "asubuhi dada" mmmhu akaguna "nzuri" akaangalia mkononi nina bahasha za kaki akajua tu ndio wale waleeeee😁😁..........mbona umekuja mapema sanaaaa ,mimi kimyaa basi akaniambia pale kama ni kazi mwaya hapa nafasi zimeisha mpka kuna watu wanajitolea bureeee,malipo yao ni chai tu na lunch basi.....daaah mpka tumbo likanisokota

Nikamwambia sawaaaa haina shida dada,nikawa naondoka mara nikasikia kwa nyuma "WAIT" tena kwa sauti kali yenye amri nikageuka nyumaaa......mmmmh huyu ni nani tena,nyie nyieeeee jamani ni mwanaume kwa makadirio anaelekea kwenye 40,kimuonekano anaonekana amechanganya asili ya nchi mbili,Africa ikiwemo ila ya pili sikuijua....nilicho note atakuwa ni mtu mwenye mamlaka ofisini hapo maana muda huo secretary alikuwa anababaika hatari mara ashike hichi mara kile .....mmmhu huyu ni nani tenaaa....mbona kabadilisha hali ya hewa hapa mpka wale wadada wa usafi wametokomeaa....hatarious!!!!!!!