Marva
Aisee mapenzi kumbe ndo yalivyo? Mbonw ham...
Aisee mapenzi kumbe ndo yalivyo? Mbonw hamkunambia kama nitazama nikasahau kabisa kazi yangu iliyonipeleka pale π₯²kazi yskuiba na kupiga pesa ...kazi yangu ya ujambazi iliyonipeleka pale....
Aah aloo nilitakiwa kuua na kuiba mavito ya thamani pale ndani kwake ....lakin guess what?
Mimi ndo niliishia kuuwawa kwa kuzama penzini na mwanaume yule , nikapagawa na u handsome wa Jasson baada ya kupewa kumbato na kiss la nguvu na yule mwanaume... π₯²
Alinivuruga ubongo wangu nikatupa bunduki chini na kutoa usirikiano aloo
Akaichapa usiku mzma π€£Palepale chumbani kwake dah sitasahau kamwe π€£ ila nili enjoy vibaya mno
Mnajua ilikuaje?ngoja niwasimulie
Mimi ni Marva ,Uzuri wangu umewahi kuwafanya wanaume wengi wapoteze mwelekeo kila wanionapo , kila nilipoonekana magari yaligongana, baskeli ziliacha njia zikaingia mtaroni , Pikipiki zilibinuka wakati mikokoteni ikiserereka mpaka sokoni
Licha ya urembo wangu pia akili yangu ndiyo iliyonifanya niogopewe hata na majambazi wakubwa. π
Sijawahi kushindwa operesheni yoyote ile .... Kila kazi niliyopewa niliimaliza kwa mafanikio makubwa .... Pale ambapo wengine walishindwa kuingia, mimi niliingia na kupiga kazi . π Pale walinzi wa benki walipoamini kila kitu kiko sawa walizubaa sana , wakati wakisinzia kwenye viti , mimi tayari nilikuwa nimemaliza kazi yangu. π° πΌ nasepa na mzigo
Sijawahi kuwa mwizi wa kawaida. Mimi ni jambazi sugu . π°π« Maisha yangu yote nimeyatumia kupanga na kutekeleza operesheni ambazo hata polisi walishindwa kuzifanikisha . π Wengi walinisikia kwa jina tu Marva Marva , lakini hakuna aliyewahi kujua sura yangu halisi. Hicho ndicho kilikuwa silaha yangu kubwa. π
Niliiba pesa nyingi mno , vito vya thamani, hati za siri na mali zilizokuwa zinalindwa kwa ulinzi mkali. ππ΅ Hakuna kitu niliyoiona ikanishinda.
Hata Mama yangu ambae alikua muuza mahindi ya kuchoma hajawahi kujua mwanae nafanya kazi gani , hata mdogo wangu Alesia hakujua kama mimi ni jambazi....
mara nyingi nikishamaliza kazi yangu nabadili nguo na kuvaa za kawaida kisha nabeba begi langu lenye vitenge vipya narudi nalo nyumbani
Nampa mama laki moja na kuendelea .....alilua akishukuru vibaya mno
Watu wengi walinijua kuwa nauza vitenge na ilikua hivyo....siku ambayo sina kazi naenda kuzungusha vitenge mtaani ....
Lakini siku moja nilipewa kazi ambayo nilidhani ingekuwa rahisi kuliko zote... Sikujua ndiyo kazi ambayo ingebadilisha maisha yangu milele. β€
Usiku huo tulikutana wote kwenye maficho yetu ya siri. π Ramani zikawekwa mezani, kila mmoja akiwa kimya akisubiri kusikia lengo la operesheni mpya. Majambazi wote tulikua wadada kasoro Pluto tu
Pluto alikua kiongozi wetu , tuliwa tumesimama kikakamavu alitutizama kisha akasema kwa sauti nzito:
"Safari hii tunamfuata bilionea mmoja na wewe Marva ndo utaenda kumaliza kazi ..." alisema
Nilitabasamu nilijua angenichagua tu
Kwangu hilo halikuwa jambo jipya. Nilipewa ramani nikaanza kuelekezwa kila kitu .nilipewa zana na kuahidi j mosi ndo siku ya kazi ...na hiyo ilikua ni j tano ......
Laiti ningejua kwamba biliome huyo angeni......
Itaendelea