kayden Mwanaume Aliyenunua Usichana Wangu
Kwenye jumba kubwa la Mr Elias zilisikiaka...
Kwenye jumba kubwa la Mr Elias zilisikiaka kelele za watu wakiwa wanabishana
"Mama siwezi tena kuvumilia Stephania amenikosea sana"
alilalamika kijana mmoja aliyeitwa Kayden
"Kayden kijana wangu watu tumeumbiwa makosa kwanini usimsamehe mwenzio nna uhakika hawezi kurudia tena"
bi Sofia alimtetea Stephania
"Hapana mama mimi siwezi tena kwasababu sio kama ni maneno ya kuambiwa bali nimeshuhudia kwa macho yangu mimi mwenyewe na hii sio mara ya kwanza kumkuta ananisaliti"
"Mama mkwe sio kweli haki ya mungu nakuapia hii ilikuwa ni mara ya kwanza na ilitokea kama bahati mbaya nakuomba uniombee kwa mume wangu anisamehe asiniache"
Stephania alipiga magoti mbele ya mama mkwe wake bi Sophia
"Wala usijali kipenzi changu nyanyuka Kayden atakusamehe na mtaendelea kuishi kama zamani"
bi Sophia alimnyanyua Stephania pale chini
"Kayden kama mimi ni mama yako basi hautamuacha Stephania"
alisema bi Sophia
"Mama Yani kabisa unamtetea mtu Baki na kumkandamiza mtoto wako mwenyewe na makosa sio yangu sijawahi kuona mama wa namna hiyo"
"Kayden unanikosea heshima unawezaje kusema maneno kama hayo"
bi Sophia alilalamika nauda huo huo mlango ulifunguliwa akaingia Mr Elias
"Kuna nini hapa kinachoendelea mana tangia naingia getini nasikia kelele zenu tu?"
Aliuliza Mr Elias
"Mume wangu, Kayden anataka kumpa taraka mke wake wewe unaona hili ni sawa kweli"
"Kayden haijalishi ni kosa gani amelifanya Stephania hauna ruhsa ya kupa taraka sijui tumeelewana"
Mr Elias alifoka
Elias alinyanyuka na kuondoka kwa hasira
"Boss tunaelekea wapi?"
Aliuliza dereva wa Kayden baada ya kupanda kwenye gari
"Turudi ofisini"
Kayden alimlaza kichwa chake kwenye huku amefumba macho ilimjia picha ya Stephania akiwa na yule mwanaume kitandani
"Benjamin badirisha ruti twende bar"
aliongea Kayden huku bado amefumba macho
Kayden
Elias ni kijana wa miaka 32 ni mtoto wa pekee katika familia ya bwana Elias na bi Sophia, Mr Elias ni tajiri mkubwa sana nchini anamilikia makampuni mbalimbali na mashule pia
Kayden hakutaka kubweteka au kurithi Mali za baba yake aliamua kupambana mwenyewe Kwa Sasa Kayden ni CEO wa kampuni yake binafsi inayoitwa NEWMILE COMPANY
"Samha ...we samha bado umelala tu mpaka saizi unategemea nani aje aoshe hivi vyombo?"
Aliuliza bi shida
"Shangazi nakuja .." samha alijivuta pale chini kwenye godoro akaamka
"Bosi ndo unaamka saizi hata wasiwasi huna mwana harmu wewe"
alifoka bi shida
"Shkamoo shangazi"
samha hakujali maneno ya shangazi yake akamslimia kwa heshima
"Sina shida ya salamu yako mimi, Yani wewe na huyo njomba Ako hamna tofauti hata kidogo wote ni mizigo kwangu"
"Unasemaje wewe mwanamke?"
Aliuliza Japhet mjomba wa samha
"Kwani nasema uongo huo ni ukweli mtupu na siku zote ukweli unauma, wewe mlevi huna mbele Wala nyuma na huyu mpwa wako ndo wale wale Hana hata kazi ya kujishikiza anasubiri shida atafute alete aweke mezani mlena kujaza choo"
bi shida aliongea kwa sauti hubwa hadi majirani walisikia
"Nitakupiga wewe mwanamke"
Japhet alimsogelea shida akampiga kibao kimoja Cha nguvu cha kwenye shavu bi shida alianguka chini akazimia
"Mjomba umeua"
samha alipiga kelele
Japhet kuona ni msala alimua kukimbilia kusiko julikaba
"Shangazi amka basi unanitisha mwenzio" samha alijaribu kumpepea bi shida
"Hembu Lete maji ataamka tu usiwe na wasiwasi kazimia tu huyu"
alisema mwanamke mmoja ambae ni jirani yao
"Sawa nitaleta"
samha aliingia ndani akatoka na sufuri iliyojaa maji wakamwagia
Na kweli aliamka
"Japhet wewe mbwa na kwamba labda usirudishe hiyo miguu yake kwenye nyumba yangu laa sivyo utaenda kunywa debe mbwa wewe"
bi shida alianzakutukana