C.E.O Woman Na Penzi La Dereva Daladala

C.E.O Woman Na Penzi La Dereva Daladala

Katika familia ya Mr Marcel na bi Rita wal...

Chapters
Chapter 1

Katika familia ya Mr Marcel na bi Rita walibahatika kupata mtoto mmoja wakike waliyempa jina la lilly , kila mtu alimuonea wivu Rita kwani mumewe Mr Marcel alikuwa tajiri na alikuwa akimpenda sana ,


ndoa yao haikudumu kwa muda mrefu bi Rita mama wa Lilly aliaga dunia kwa maradhi ya kansa alimuacha binti yake lilly akiwa na miaka 13 tu

" Tumeshamaliza msiba Sasa itakuwaje kuhusu Lilly?"

Aliuliza shangazi yake lilly bi Eva


" Sijui kama nimekuelewa au laa lakini ninachoweza kukwambia ni kuwa naweza kumlea vizuri tu binti yangu sitaki msaada kutoka kwa mtu yoyote "

alisema Mr Marcel

" Mmh mimi nakujua vizuri kaka yangu ndomana nilikuwa nakushauri uoe ili lily apate malezi Bora muda wote upo busy na kazi utamuangalia saa ngapi mtoto au utawaachoa wafanyakazi"

alisema Eva

" Eva naomba unyamaze huoni hata aibu ndo kwanza tumemaliza msiba unataka nikaoe mwanamke mwingine "

alifoka Marcel kisha alinyanyuka na kuingia ndan

i " Utaoa tu nakwambia utake usitake na mwanamke wa kuoa tumeshakuchagulia "


Eva aliondoka

" Daddy Ina maana mama ndo hayupo tena ?"

Lilly alikuwa haamini amini kile kinachoendelea


" Ndio hatunae tena ngoja akapumzike ameteseka sana , nakuhakikishia nitakupa upendo wa hali ya juu na zaidi ya ule tuliokupa zamani mimi na mama yako "

alisema Mr Marcel


" Asante sana Dady na mimi nakuahidi wewe na mama yangu aliyetangikia kuwa nitakuwa binti mzuri na mwenye mafanikio makubwa "


alisema lilly huku anatabasamu

" Najivunia sana kuwa na binti kama wewe hata mama yako huko aliko atakuwa anajivunia sana kuwa na binti kama wewe "


Mr Marcel alimkumbatia binti yake lilly ,


Baada ya week moja kupita lilly alirudi shuleni , ilikuwani shule ya bweni alikaa huko kwa miezi mitatu bila kurudi nyumbani aliwasiliana tu na baba yake kupitia simu Muda wa likizo ulifika Lil


ly alirudi nyumbani alishangaa kukuta mazingira yapo tofauti na alimkuta mwanamke mmoja alionekana kama mama mwenye nyumba maana aliwafokea wafanyakazi na kuwatuma atakavyo


" Shkamoo Dady "


Lilly alimsalimia baba yake Mr Marcel na kumpuuzia yule mwanamke

" Marahaba , Lilly mbona upo hapa kwani ni kipindi Cha likizo ?"


Mr Marcel alimuuliza binti yake lilly


" Daddy kweli umesahau kila kitu nadhani nilikwambia Leo ni siku yetu ya kufunga shule "


lilly aliongea kwa kudeka kwa baba yake "


Oh samahani kipenzi changu unajua mambo mengi nilisahau kabisa "


Mr Marcel aliongea huku anakuna kichwa chake


" Na huyu mwanamke ni nani naona anafokea wafanyakazi bila mpangilio wowote ?"


Lilly aliamua kumuuliza baba yake Mr Marcel alimuangalia yule mwanamke aliyekaa pembeni yake kisha akamgeukia lilly



kabla hajaongea chochote
waliingia watoto wawili wakike na wakiume walionekana kama mapacha

" Shkamoo baba , shkamoo mama"

walisalimia wale watoto walikuwa wakubwa kidogo kwa Lilly


"Marahaba watoto wangu wazuri vipi maendeleo yenu ya shule ?"


yule mwanamke alienda kuwa kumbatia wale watoto


" Yako vizuri Leo tunaanza likizo yetu tunataka kwenda kwa babu "


walisema wale watoto

Lilly alibaki kumkazia macho baba akiwa anasubiri jibu la swali lake kwa hamu


" Lilly huyu anaitwa bi Rhoda ni mama yako wa kufikia na Hawa wawili ni kaka yako na dada yako John na johari"


Mr Marcel alitoa utambulisho


" Wow kumbe wewe ndo mdogo wetu karibu sana nyumbani "

John alimkaribisha lilly , kwa upande wa johari alimuangalia Lilly kwa dharau kisha aliondoka


" Hii haipo sawa kabisa Dady ni miezi michache imepita tangia mama atuache imekuwaje tayari unafamilia tena unaishi kwa furaha kama hakuna chochote kilichotokea , vipi kuhusu mimi ?"


lilly aliongea kwa uchungu huku machozi yanamtoka kwenye macho yake mazuri


" Lilly wewe ni binti yangu lakini hauruhusiwi kuvuka mipaka yako unawezaje kumfundisha baba yako nini Cha kufanya ondoka nenda chumbani kwako haraka "


mr Marcel alifoka


"Okay nitaondoka mbele ya macho yako naona siku hizi sina thamani tena kwako "


lilly alikimbilia chumbani alifungua mlango lakini hakuingia alibaki amesimama mlangoni


" Wewe kwanini upo chumbani kwangu ?"


Lilly alimuuliza johari aliyekuwa busy kupaka rangi kucha zake


" Oh masikini baba yako hakukwambia hiki ni chumba changu unaweza kwenda kumtumia chumba kingine utakachokipenda "


johari aliongea kwa dharau akapiga teke begi la lilly likaanguka chini ,lilly alijikuta miwili wote unaishiwa na nguvu


" Mume wangu huyu binti yako mbona kama tutashindwana siku ya kwanza tu kurudi ananiita mimi mwanamke kashindwa hata kusema shangazi kama hawezi kuita mama "


bi Rhoda alilalamika kwa Mr Marcel


" Aaah usijali mke wangu si unajua mwanzo alikuwa mwenyewe alikuwa ana deka sana lakini saizi anawenzie itabidi ajifunze na akubali kila alichokikuta "

alisema Mr Marcel

Muda huo huo lilly alishuka akiwa analia


" Vipi mbona unalia ?"


Mr Marcel alimuuliza binti yake lilly

" Daddy kwanini chumba alichonitengenezea mama yangu anakitumia yule msichana nataka atoke kwenye chumba changu Sasa ivi "

lilly aliongea huku analia


" Kuwa na adabu binti yule si ni dada yako kwanini umnyanganye chumba? vyumba vingine kwani havipo "

bi Rhoda alimfokea lilly mbele ya baba na baba yake hakufanya chochote Kwanzia siku hiyo maisha ya lilly yalikuwa ya kunyanyasika na baba yake alihisi kama lilly ni muongo na hakuna ukweli wowote



" Daddy laptop yangu imeharibika naomba uninunulie nyingine "

lilly alimwambia baba yake


" Sawa nitakununulia "


Mr Marcel alikubali muda sio mrefu Johar nae alienda kumuomba Mr Marcel baba yake wa kufikia amnunulie laptop pia

" Baba laptop yangu haiwaki sijui shida ni nini naomba uninunulia nyingine "


Johar alimwambia Mr Marcel

" Sawa usijali , Leo jioni nitarudi na laptop mpya kwaajili yako"

Mr Marcel alimnunulia laptop Johar na kumuacha Lilly mpaka alimkumbusha kwa mara nyingine Maisha ya Johar yalikuwa ya kushindana na lilly atakachokitaka au kupata lilly na yeye pia anataka akipate pia


Baada ya miaka mitano kupita lilly akiwa na miaka kumi na nane alikutana na kijana mmoja aliyeitwa Amir walianzisha mahusiano

baada ya johari kulijua Hilo alitamani sana siku moja aje kumpata Amir kama kumkomoa lilly

" Wanajikuta wanapendana sana subiri nitafanya kila njia ili nimpate huyu mapenzi wako "


Johar aliongea huku anacheka kisha alienda kwa baba yao Mr Marcel


" Baba nilikuta hiki kikaratasi kwenye begi la lilly "....


Johar alimpatia kile kikaratasi Mr Marcel ilikuwa ni barua ya mapenzi

" Umezikuta wapi umesema ?"


Mr Marcel aliuliza kwa ukali


" Sasa ndo unamuulizaje kwa ukali hivyo , mtoto amekuletea barua anasema kazikuta chumbani kwa lilly wa kufokewa hapa ni lilly na sio Johar wangu "


alisema bi Rhoda


" Kaniitie lilly mwambie afike hapa haraka "

.Mr Marcel alikasirika sana...


" Wewe kizuu baba yako anakuita huko

" johari alimwambia lilly


" Nakuja na ukome kuniita kizuu kama mimi kizuu basi wewe ni ndondocha mana kila siku repoti zikija wa pili kutoka mwisho Bora hata John anajitahidi kuliko wewe "

lilly alimzomea johari kisha alimpita na kwenda sebleni

" Daddy nimesikia unanita .."

. lilly hakuwa amekaa sawa alikaribiswa na Kofi zito la kwenye shavu alianguka mpaka chini


" Daddy nimefanya nini, mbona unanipiga ?"

Lilly alishika shavu lake huku analia


" Huu ndo ujinga unaoufanya si ndio ame kweli mtoto wa kike anachukua tabia za mama yake "

bi Rhoda alimtupia lilly zile barua pale chin

i " Usimuingize mama yangu kwenye makosa yangu "

lilly alimkata jicho bi Rhoda

" Naona umekubali makosa yako Sasa kwanzia leo sitaki kukuona nyumbani kwangu "


alifoka Mr Marce

l " Sasa nitaenda wapi daddy ?"

Lilly alipiga magoti mbele ya baba yake Bi Rhoda na johari walifurahi kusikia hivyo

" Kusanya nguo zako usisahau na passport unaenda marekani utasomea huko sitaki kusumbuliwa kichwa changu kina mambo mengi sana ya kufanya "

Mr Marcel alinyanyuka na kuelekea chumbani kwake

" Mama Sasa mbona kama anaenda tena marekani ku enjoy maisha na mimi sikupanga iwe hivyo "

johari alimwambia mama yake mbele ya lilly Wala hakuona haya


" Usijali kipenzi kila kitu kina muda wake "


bi Rhoda alimshika mkono johari wakaondoka walimuacha lilly pale chini analia kwa uchungu alijikuta anamkumbuka sana mama yake


" Mama umenicha mkiwa sina pa kukimbilia ni Bora ungenichukua na mimi tukaenda wote "


lilly alilia kwa uchungu wafanyakazi walimuonea huruma lakini hawakuwa na Chochote Cha kumsaidia