C.E.O NA EX WANGU

C.E.O NA EX WANGU

Mi bwana naitwa martha ni single mother . ...

Chapters
Chapter 1

Mi bwana naitwa martha ni single mother .
  Mimi nilipata mtoto wangu wa kwanza nikiwa form two tu. nikapata huyo mkaka alikuwa chuo yeye anaitwa Bosco .

  Bosco hakuwa mwanaume wangu wa kwanza lakini  mimi namuhesabu kama wa kwanza kwa sababu  ndie mwanaume ambae nilimpenda kupita  maelezo yaani ndo mwanaume ambae alinifanya nikajua hasa mapenzi ni ninii.

    Nyuma niliwahi kuwa na wanaume wawili kwa wakati tofauti nakumbuka nikiwa darasa la saba ndo nilianza mahusiano na ka kijana kamoja tunasoma nako sema yeye alikiwa B mi A hata sijui ilikuwaje aisee  nikajikuta tu nishalala nae usichana tena sina na baada ya mahafari na fukafanya mtihani ndo tukapoteana hivyo hata sikuwahi kabisaa kumfikiria  yaani ukisikia mchumba wangu wa darasa la saba basi ndo huyo lakini sijawahi kumtafuta wala sina shida nae ..

   Nilipo ingia form one,Kuna mkaka alikuwa ananitaka sana yeye alikuwa form two,Sijui hata nae ilikuwaje bana et akawa bwana wangu dah, yaani nilikuwa kama zoba zoba sijui kusema sitaki au hapana, sijui nilikuwa nawaonea huruma mie hata sijui kwakwel ila ninacho jua mi sio malaya .

    Nilipo ingia kidato cha pili siku moja  tulienda kwenye mechi shule flan hivi ya jeshi ipo mbali tu na shuleni kwetu .

   Siku hiyo ndio  nilikutana na Bosco yeye alikuwa  Chuo mwaka wa pili   ,Hiyo siku walikuja na marafiki zake nao kuangalia mechi uwanja tulio kuwa tunachezea sio mbali na  hostel  zao zilipo ..

    Akaniomba namba ukweli  kuanzia hiyo siku nilijikuta silali kabisa namuwaza yeye tu usiku ulikuwa mrefu sanaa . Akinichatisha yaani nasikia rahaaa mnoo naweza  hata kumbatia simu naona kama nina bahati njemaa .

  Siku alipo nitongoza aisee😅 nilitanani hata kuita waandishi wa habari waje kunihoji kwanzaa🙌😅 nikasema ndio bila hata kufikiria mara mbili na nikakana kabisa sina mahusiano na ukumbuke hapo nilikuwa natoka na yule mkaka wakati  huo alikuwa form three mimi form two😄 ila nikasema sijawahi kuwa na mahusiano  si akajua mi bikra😅

   Nilikuwa chizi kwa huyu kaka kwanza alikuwa handsome halafu msafii ananukia huyoo. Ana akili hatari mimi nikaamini huyu ndio mume wangu .

Nilikuwa namuheshimu namtii 🙌 nikavunja mahusiano na yule kaka wa  mwanzo ili niwe huru .

   Bosco hata aseme anashida na mimi sa 8 usiku walai nitaamka kwenda , Kwenye panzi lake sikuona hatari yeyote kama hatari ya kumpoteza , Nilimpenda huyu kaka  nikampenda tenaa ilikuwa hata nikimeza mate yanachora jina lake we huogopi, mi naogopa😅😅

    Mahusiano yangu yalinoga miezi minne tu yaani ndani ya miezi minne Bosco alikuwa ananidekeza hatarii japo hakuwa ananipa hela... tangu nimekuwa nae mpaka tunaachana pesa aliyonipa ni 10000 tu ya kitanzania yaani ndo hela yake niliyokula tena kuna siku alinipa 2000 akaja kunipa 3000 na mara mwisho nilipo mwambia nina mimba akanipa 5000 nikanunue dawa niitoe😅😅 sasa hivi nacheka kama mazuri kaka alijua kunitesa huyu ila sikuwa naweza kabisaa ku move on , Hakuna Rangi ambayo sijaona jamani  hakuna kilio sijalia mie kulilia hili penzi 🙌

    Miezi minne ilitosha kabisa kunifanya nikalili nyimbo zote za Shelkan😅 niliona penzi langu hata hao wahindi wanaiga kwetu , baada ya hapo aloo  nilirudi kumsikiliza  Lava lava hata yeye niligundua hajui bado kuumizwa na mapenzi  huyu hajui kabisa maumivu niliyoyapata aah lava haingii kwanguu ..

Nikajichanganya nikabeba mimbaa hii ilikuwa ya bahati mbaya hata mimi sikuwa nimetarajiaa nyiee😭😭 mwanaume alinambia toa mimba mi siwezi kuzaa na mwanamke  hana akili shulee ananitamkia bila hata aibuu jamanii😭 Niliumia sana kweli sikuwa na akili shule mimi mwenyewe nimelelewa na single mother, Kwa habari za mama ni kwamba  baba alikata  mimbaa na akamwambia aitoe akakataa ,mama alikuwa mfanyakazi tu wa ndani kwahiyo mimba ilikuwa ya boss wake ..

   Amepambana leo bint mkubwa na mie narudia yale yalee😭 Mama alivyojua nina mimba alivunjika sana moyo ila hakunipiga wala kunifokea akaniuliza tu baba wa mtoto yupo wapi nikamwambia amenipa hela nikatoe ,Mama anaiomba hiyo hela nampa elfu 5😅😅 kwanza alicheka Elfu 5 ndo yakutolea ujauzito?? .

  Basi mama akachukua namba yake akampigia Bosco alinikana kabisaaa et nina wanaume wengi  sana hiyo mimba sio yake nyie  huyu kaka nilimpendaaa aisee ila ndo kanivunja vunja kabisaaa ..

Mama akanambia achana nae utazaa shule kwenyewe ulikuwa unaenda tu kupoteza muda achana nao basi nikasema sawa .

Ila sikuachana na Bosco kila siku nilikuwa naenda kwake namliliaaa😅 tuendelee na penzi yaani sikuweza kuchomoa kwa huyu kaka jamani sina pawa , dharau sasa mjinga yule et ananambia kama unataka kuendelea na mimi toa huo ujauzito 🙌 nilitamani kutoa ili tuendelee na nilijaribu mara mbili eeh mwanangu nisamehe mimi nisamehe sana kipenzi changu nilikuwa kipofu hata nikataka ufe wewe ili kuifurahusha nafs ya fala mmoja tu 🙌 huwa najutia sana huko kitu .. 

    Nilijifungua jamani mtoto coppy ya yule kakaa nikajua hapa atanipenda tena. mtoto wa kiume haloo🥰🥰  nikampa taarifa  ya kujifungua akanambia tu Hongera 🥹🥹 yaani kawaida tu niliumia ila nikapotezea , Ile nimetoka tu 40 nikabeba mtoto labda alimuona walivyo fanana atakubali aah wapiii jamani huyu kaka alinitukana akasema yeye hana mtoto. Mtoto wake nilisha toa kwenye ile hela aliyonipa ..

Nilirudi nyumbani   nililiaa. Nililia kuliko  hata mwanangu  mwenyewe 🥹🥹 mama alinisema sana kwanini nimeenda huko akanikanya niendelee na maisha yangu niachane naee !!

  Yaani mama anavyoongea kurahisi kwelii hivi anajua mapenzi huyu kweli?? Sidhani kama aliwahi kupenda maana hata baba nahisi alimtumia kwa nguvu tu🥹🥹

  Basi Tarabibu  niliendelea na maisha yangu japo mwanzo nilikuwa simpendi sana mwanangu yaani nilijikuta namchukiaa kweli kweli naona kama balaa tu kwangu ..

  Mama ndo alikuwa kama mtoto wake mie hata kumnyonyesha mpaka nilazimishwe. Nyie mapenzi Dah  nikikumbuka  nabaki tu kumshukuru mungu kile kipande nilivuka salama kabisaa  na leo  nimesimama

Ilinichukua muda sana ku move on siwezi kuelezea yotee ila nimepita nikasimama upyaa ..

Ila habari za mapenzii aisee habari  za mapenzi  hee!! Yaani ukitaka kupandisha mashetani yangu aloo nitongoze wee nakuwa kichaa mimi  hakuna Tusi utaacha kuliona kwangu  loo...

ITAENDELEA...